

Lugha Nyingine
Meli kubwa ya utalii ya kwanza kuundwa na China yaondoka kwenye gati katika Mji wa Shanghai
![]() |
Picha hii iliyopigwa Juni 6, 2023 ikionyesha meli kubwa ya utalii ya kwanza kuundwa na China "Adora Magic City" katika Mji wa Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Ding Ting) |
SHANGHAI - Meli kubwa ya utalii ya kwanza kuundwa na China imekamilisha kuondoka kwake kutoka kwenye gati huko Shanghai siku ya Jumanne, ikionesha kuhamishwa kwake kikamilifu kwenye hatua ya kuingia majini kutoka kwenye gati.
Meli hiyo ya utalii inayoitwa "Adora Magic City," inatarajiwa kukamilika na kukabidhiwa rasmi mwishoni mwa mwaka huu wa 2023.
Hadi kufikia sasa, zaidi ya asilimia 93 ya uundwaji wake na zaidi ya asilimia 85 ya kazi zake za ndani zimekamilika, kwa mujibu wa Kampuni ya Uundaji Meli ya Shanghai Waigaoqiao ya Kundi la Viwanda vya Uundaji Meli la China (CSSC).
Meli hiyo ya utalii, yenye urefu wa mita 323.6 na upana wa mita 37.2 na jumla ya uzito wa tani 135,500, ina uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 6,500. Itakuwa na hoteli ya kifahari, kumbi za sinema na bustani ya maji ndani yake.
"Meli ya utalii itaondoka kutoka Shanghai kuelekea Japani na Asia ya Kusini-Mashariki baada ya kukamilika kuundwa na kukabidhiwa. Njia yenye umbali wa kati na mrefu kwenye Njia ya Hariri ya Baharini itaanzishwa kwa wakati ufaao," amesema Roger Chen, Mkurugenzi Mkuu wa CSSC Carnival, kampuni ambayo itakuwa mwendeshaji wa meli hiyo.
Uundaji wa meli kubwa ya utalii ya pili ya China ulianzia Agosti 2022.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma