China yarusha chombo cha kubeba mizigo kwenye kituo cha anga ya juu cha China cha Tiangong

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 11, 2023
China yarusha chombo cha kubeba mizigo kwenye kituo cha anga ya juu cha China cha Tiangong
Roketi ya Long March-7 Y7 iliyobeba chombo cha mizigo cha Tianzhou-6 iliruka ilirushwa kutoka kwenye Eneo la Urushaji Vyombo kwenye Anga ya Juu la Wenchang katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Mei 10, 2023. (Xinhua/Yang Guanyu)

WENCHANG, Hainan - Shirika la Anga ya Juu la China limesema, China siku ya Jumatano usiku imerusha kwenye anga ya juu chombo cha kubeba mizigo ili kusafirisha vifaa kwenye kituo chake cha anga ya juu cha Tiangong kinachozunguka.

Ikiwa imebeba chombo cha mizigo cha Tianzhou-6, roketi ya Long March-7 Y7 ilipaa juu majira ya saa 3:22 usiku (Saa za Beijing) kutoka Eneo la Urushaji Vyombo kwenye Anga ya Juu la Wenchang katika mkoa wa kisiwa wa Hainan, shirika hilo limesema.

Baada ya dakika 10 hivi, Tianzhou-6 ilijitenga na roketi na kuingia kwenye obiti yake maalum. Upesi paneli zake za jua zilifunuliwa na kuanza kufanya kazi. Shirika hilo limetangaza urushaji huo kuwa wenye mafanikio kamili.

Chombo hicho za mizigo baadaye kitafanya minyumbuliko ya kiotomatiki na kutia nanga na kuungana na kituo cha Tiangong katika obiti.

Chombo hicho cha Tianzhou-6 kilichorushwa kimeboreshwa vipengele ikilinganishwa na ufundi wa awali wa Tianzhou, kikiwa na ujazo mkubwa wa upakiaji na uwezo mkubwa wa kubeba.

Wang Ran, mbunifu mkuu wa mfululizo wa vyombo vya Tianzhou ambaye anafanya kazi ya ushirikiano na Idara ya Utafiti wa Teknolojia ya Anga ya Juu ya China, amesema kiwango cha upakiaji kinachofaa kiliongezeka kutoka mita za ujazo 18.1 hadi mita za ujazo 22.5, sawa na upanuzi wa asilimia 20. Uwezo wa kupakia umeboreshwa hadi tani 7.4, na kukifanya Chombo cha Tianzhou-6 kuwa chombo kikubwa zaidi cha kubeba mizigo duniani katika huduma.

Katika safari hii ya kwenye anga ya juu, Chombo cha Tianzhou-6 kimebeba vitu mbalimbali zaidi ya 200, vikiwemo vifaa vya kila siku vya wanaanga pamoja na nguo, chakula, matunda na maji, vyote vikiwa na uzito wa jumla wa karibu tani 5.8.

Chombo cha Tianzhou-6 pia kimepewa jukumu la mradi wa majaribio wa satelaiti wa Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Dalian.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha