Vifaa vinavyotumia Teknolojia za Akili Bandia (AI) vyaongeza ufanisi wa ufugaji wa ng'ombe wa maziwa huko Wuwei, Kaskazini mwa China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 09, 2023
Vifaa vinavyotumia Teknolojia za Akili Bandia (AI) vyaongeza ufanisi wa ufugaji wa ng'ombe wa maziwa huko Wuwei, Kaskazini mwa China
Mfanyakazi akijulisha mfumo wa teknolojia za akili bandia wa usimamizi kwenye shamba la kukamua na kusindika maziwa huko Wuwei, Mkoa wa Gansu, Kaskazini-Magharibi mwa China, Mei 7, 2023. (Xinhua/Ma Xiping)

Vifaa vinavyotumia teknolojia za akili bandia (AI) vimeongeza ufanisi wa shamba, na kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa mifugo kuwa sahihi zaidi.

Mkufu wa ufuatiliaji uliowekwa kwa kila ng'ombe hukusanya data nyingi za mifugo kama vile pumzi, mwenendo wa kucheua, hali ya kulisha na idadi ya hatua. Data hizi hupitishwa kwa wakati halisi kwa madaktari wa mifugo ambao wanaweza kufuatilia ukamuaji wa maziwa kutoka kwa ng'ombe na hali za kiafya.

Zaidi ya hayo, lebo za kielektroniki za sikio hutoa njia rahisi ya kutambua na kudhibiti ng'ombe mmoja mmoja, sawa na kumpa kila ng'ombe kitambulisho. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha