

Lugha Nyingine
China yafanya Mkutano wa 6 wa Kilele wa Kidijitali ili kuhimiza maendeleo ya kidijitali
FUZHOU - Mkutano wa 6 wa Kilele wa Kidigitali wa China umefunguliwa Alhamisi katika Mji wa Fuzhou wa Mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China.
Li Shulei, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC, alitoa hotuba muhimu kwenye ufunguzi wa mkutano.
Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma wa China Leung Chun-ying pia alihudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano huo.
Mkutano huo wa kilele wa siku mbili unalenga kuonyesha mafanikio mapya ya Mpango wa Kidijitali wa China, na kubadilishana uzoefu katika maendeleo ya kidijitali.
Washiriki wamepata fursa ya kushuhudia maendeleo ya ajabu katika maeneo kama vile miundombinu ya kidijitali, uchumi wa kidijitali na jamii ya kidijitali katika maonyesho mahsusi kwa ajili ya maendeleo ya kidijitali.
Maonyesho ya bidhaa za kidijitali, mashindano ya uvumbuzi wa kidijitali na majukwaa mfululizo pia yamepangwa kufanyika wakati wa tukio hilo.
Mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja na Idara ya Usimamizi wa Mtandao ya China, Kamati ya Kitaifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China, Wizara ya Sayansi na Teknolojia ya China, Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari ya China, Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Mali ya Kitaifa ya Baraza la Serikali la China, pamoja na Serikali ya Umma ya Mkoa wa Fujian.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma