

Lugha Nyingine
China yatoa picha zenye rangi za Sayari ya Mars (3)
![]() |
Picha hii iliyotolewa Tarehe 24 Aprili 2023 ikionyesha ramani ya Mercator pamoja na ramani ya azimuthal ya Sayari ya Mars. (CNSA/ Xinhua) |
HEFEI – Idara ya Kitaifa ya Anga ya Juu ya China (CNSA) na Taasisi Kuu ya Sayansi ya China kwa pamoja zimetoa picha mfululizo za Sayari ya Mars zilizopatikana wakati wa safari ya kwanza ya China ya utafiti wa Sayari ya Mars, picha hizo ambazo watu wa dunia nzima wanaweza kuziona.
Picha mfululizo zenye rangi zimetolewa kwenye hafla ya ufunguzi wa Siku ya Anga ya Juu iliyofanyika Hefei, Mji Mkuu wa Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China.
Zikiwa zimeandaliwa kwa kufuata viwango vya ramani na mwonekano wa anga wa mita 76, picha hizo ni pamoja na picha za ramani sanifu za nusu Sayari ya Mars ya mashariki na ya magharibi, Ramani ya Robinson ya Sayari ya Mars, na Ramani ya Mercator pamoja na Ramani ya azimuthal ya sayari hiyo.
Kwa mujibu wa CNSA, picha hizi zinatokana na data ya picha 14,757 zilizopatikana kupitia kamera inayohisi kwa mbali kwenye obita ya Chombo cha Anga ya Juu cha China cha Tianwen-1 kwa muda wa miezi minane kuanzia Novemba 2021 hadi Julai 2022.
Chombo cha anga ya juu cha China cha Tianwen-1, kinachojumuisha obita, lander na rover, kilirushwa kwenye anga ya juu Julai 23, 2020 na kuingia kwenye mzunguko wa Sayari ya Mars baada ya siku 202 za kuruka.
"Picha za kimataifa za Sayari ya Mars zitatoa ramani ya msingi bora zaidi kwa ajili ya uchunguzi wa Sayari ya Mars na utafiti wa kisayansi," amesema Zhang Rongqiao, mwandaaji mkuu wa safari ya kwanza ya China ya uchunguzi wa Sayari ya Mars.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma