

Lugha Nyingine
China yarusha roketi mpya ya kubeba setilaiti kwenda anga ya juu
(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 03, 2023
JIUQUAN - Roketi mpya ya kubeba setilaiti na vifaa mbalimbali kwenda anga ya juu imefanya safari yake ya kwanza nchini China siku ya Jumapili, na kutuma satelaiti kwenye mzunguko wake uliopangwa.
Roketi hiyo inajulikana kwa jina la TL-2 Y1 na iliruka kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan Kaskazini-Magharibi mwa China saa 10:48 Jioni. (Kwa muda wa Beijing).
Setilaiti hiyo imepangiwa kazi za kuthibitisha mpango wa jumla wa roketi na uratibu kati ya mifumo na kupata vigezo vya mazingira ya kujongea kwa chombo
Pia itatumika katika majaribio ya kuhisi kwa mbali na kupata picha za kidijitali na uthibitishaji mwingine wa kiufundi.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma