Mkoa wa Guangdong China waharakisha mageuzi ya teknolojia za akili bandia na za kidijitali za viwanda
 |
Picha hii iliyopigwa Tarehe 20 Machi 2023 ikionyesha karakana ya Kampuni ya Kuunada Magari ya GAC Motor huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. Katika miaka ya hivi karibuni, Mkoa wa Guangdong umeharakisha mageuzi ya teknolojia zinazotumia akili bandia na za kidijitali katika viwanda vya utengenezaji bidhaa ili kukuza maendeleo yenye ubora wa juu.
Hadi kufikia sasa, kuna kampuni zenye kuendesha viwanda zinazofikia 67,000 kwenye kiwango kilichopangwa hapo awali na kampuni zinazotumia teknolojia ya juu zimefikia 69,000 katika mkoa huo. (Xinhua/Deng Hua) |
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)