Meli kubwa nyingine ya kimataifa ya usafirishaji nishati yakabidhiwa Qingdao, China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 08, 2023
Meli kubwa nyingine ya kimataifa ya usafirishaji nishati yakabidhiwa Qingdao, China
(Picha ilipigwa na Zhang Jingang/People's Daily Online)

Uundaji wa moduli kuu mbili za mwisho za vifaa vingine vikubwa vya kimataifa vya kusafirisha nishati, ambavyo ni vya mradi wa Gesi asilia ya Kimiminika (LNG) wa Canada zilizojengwa na Kampuni ya Mradi wa Mafuta Baharini ya China zilikamilika na kupakiwa kwenye meli tarehe 7 huko Qingdao, China. Hadi hivi sasa, moduli zote zilizoundwa na upande wa China zimekabidhiwa vizuri.

Habari zinasema, mradi huo ni mradi wa LNG wa kimataifa unaowekezwa na kampuni tano kuu za mafuta duniani, ikiwemo kampuni ya Shell. Katika kipindi cha kwanza cha ujenzi wa mradi huo, mistari miwili ya uzalishaji imepangwa kujengwa, ambayo itakuwa na uwezo wa kuzalisha LNG tani milioni 14 kila mwaka. Baada ya mistari hiyo miwili kukamilika, itatoa nishati safi ya ubora kwa China na nchi nyingine za Asia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha