

Lugha Nyingine
Waendeshaji wanawake wa droni wanyunyiza matumaini juu ya mashamba Hubei, China (5)
Mnamo mwaka 2015, Jiang Minglan aliyefanya kazi ya kuhifadhi mimea kwenye Tianmen, Mkoa wa Hubei wa China, alipata fursa ya kuona droni ya kuhifadhi mimea , akaiingiza na kuitembeza. Baadaye, alijumisha kikundi cha waendeshaji kumi wa droni kumi za ulinzi wa mimea.
Mwaka 2019, chini ya unngaji mkono wa Shirikisho la Wanawake, kikundi chake kilitoa mafunzo kwa wanawake waliobaki kijijini huko Tianmen. Waliunda timu ya wanawake ya kuhifadhi mimea kwa droni ili kutoa huduma kwa wakulima wanaohitaji kupanda mbegu au kunyunyiza dawa, na pia kuwasaidia wanawake hao kuongeza kipato chao.
Hivi sasa, timu hiyo imetoa mafunzo kwa wanafunzi wanawake zaidi ya 300, miongoni mwao kuna waendeshaji rasmi wanawake 37, ambao wanaweza kuendesha droni zao ziruke mbali zaidi hata mpaka Mkoa wa Henan na Mkoa wa Xinjing wa China.
Picha inapigwa na Xiao Yijiu/Xinhua.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma