Mkutano wa Kimataifa wa Simu za Mkononi wa Mwaka 2023 washuhudia kurejea kwa nguvu kwa washiriki wa Bara la Asia (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 28, 2023
Mkutano wa Kimataifa wa Simu za Mkononi wa Mwaka 2023 washuhudia kurejea kwa nguvu kwa washiriki wa Bara la Asia
Mtembeleaji wa maonyesho akijaribu kifaa cha Uhalisia Pepe katika Mkutano wa Kimataifa wa Simu za Mkononi wa Mwaka 2023 mjini Barcelona, Hispania, Februari 27, 2023. (Xinhua/Meng Dingbo)

BARCELONA, Hispania - Mwandalizi wa shughuli kubwa zaidi ya kila mwaka ya Barcelona amesema, Mkutano wa Kimataifa wa Simu za Mkononi wa Mwaka 2023 (MWC) umeanza Jumatatu huko Barcelona ukipata nguvu kubwa zaidi kutokana na kurejea kwa washiriki wa Bara la Asia.

Mratibu wa mkutano huo Shirika la GSMA limesema, kati ya watu wapatao 80,000 kutoka zaidi ya nchi na maeneo 200 wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo, watu wapatao 5,000 wameandikishwa kutoka China, baada ya nchi hiyo ya Asia kuondoa vizuizi vya kusafiri mapema mwaka huu.

Mkutano huo wa Kimataifa wa Simu za Mkononi wa Mwaka 2023 (MWC) ambao utashirikisha makampuni na mashirika zaidi ya 2,000 kuonyesha bidhaa zao mpya ili kuonyesha uvumbuzi wa teknolojia mpya katika tasnia ya simu, utaendelea hadi Alhamisi wiki hii. Mkutano huo pamoja na maonyesho yake utafanyika katika kituo cha maonyesho cha Fira Gran Via.

Wakati huu kampuni za China kama vile Honor, Xiaomi na OnePlus, na vile vile Nokia, zitazindua simu mpya kadhaa, zikiwemo simu zinazoweza kukunjwa na zinazochaji haraka. Nafasi ya soko ya kampuni kubwa ya teknolojia ya China Huawei imeongezeka kwa asilimia 50 zaidi ya mwaka jana.

Kwa mujibu wa waandaaji, mkutano huo na maonyesho yake wenye kaulimbiu inayojikita kwenye “Kasi ya Mtandao”, utajumuisha semina tano muhimu zinazolenga kuongeza kasi ya 5G, Uhalisia+, MtandaoWazi, Fedha Kidijitali na Maisha ya Kidijitali katika kila kitu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha