Mji wa Busan, Korea Kusini waandaa maonyesho makubwa zaidi ya droni barani Asia (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 24, 2023
Mji wa Busan, Korea Kusini waandaa maonyesho makubwa zaidi ya droni barani Asia
Picha hii iliyopigwa Februari 23, 2023 ikionyesha droni inayoonyeshwa kwenye Maonyesho ya Droni ya Korea Kusini Mwaka 2023 katika Kituo cha Maonyesho na Mikutano cha Busan huko Busan, Korea Kusini. (Xinhua/Wang Yiliang)

BUSAN, Korea Kusini - Mji wa bandari wa Kusini-Mashariki mwa Korea Kusini wa Busan unaandaa maonyesho makubwa zaidi ya droni barani Asia ili kuonyesha teknolojia na modeli mpya zaidi za kisasa za sekta hiyo, serikali ya mji huo imesema Alhamisi.

Maonyesho ya Droni ya Korea Kusini Mwaka 2023, ambayo ni ya saba ya aina yake, yamepangwa kufanyika kwa siku tatu hadi Jumamosi kwenye Kituo cha Maonyesho na Mikutano cha Busan (BEXCO).

Kwa kile ambacho mji umesema ni maonyesho makubwa zaidi ya droni barani Asia, mabanda 625 yanayohusisha kampuni 172 yamepangwa katika ukumbi huo wa maonyesho wenye ukubwa wa mita za mraba 17,600.

Chini ya kaulimbiu isemayo "Kila kitu kuhusu droni, Mustakabali wetu na wa droni", maonyesho hayo yatatilia maanani uboreshaji wa sekta ya droni huku yakianzisha ufundi wa mafungamano ya sekta hiyo na modeli na miundo mbalimbali ya droni.

Maonyesho hayo yanakutanisha kwa pamoja kampuni zinazoongoza kutoka sekta mbalimbali za teknolojia, ikiwa ni pamoja na mawasiliano ya simu, uongozaji wa safari kwenye nafasi ya kijiografia, akili bandia (AI) na kujifunza kwa mashine, Mtandao wa Mambo (IoT), na roboti.

Kampuni za kimataifa, ambazo zilikuwa na ugumu wa kushiriki maonyesho hayo kutokana na janga la UVIKO-19, sasa zimeshiriki katika shughuli ya mwaka huu. Zinajumuisha kampuni kama vile Kampuni ya Betri ya Shenzhen Grepow, Shenzhen Vigorpower na DJI kutoka China, Liberaware na Amuse Oneself kutoka Japani na Flyability SA kutoka Uswizi.  

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha