Basi linalotumia teknolojia za Akili Bandia lafanya majaribio ya kuendeshwa barabarani Xiongan, China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 23, 2023
Basi linalotumia teknolojia za Akili Bandia lafanya majaribio ya kuendeshwa barabarani Xiongan, China
Basi la majaribio linalotumia teknolojia za akili bandia la njia ya mstari wa 901 likipita kwenye taa za kuongoza watumiaji wa barabara Tarehe 22, Februari. (Picha na Chinanews)

Basi linalotumia teknolojia za akili bandia la Eneo Jipya la Xiongan huko Baoding, Mkoa wa Hebei wa China kwa sasa linafanyiwa majaribio ya kuendeshwa barabarani kabla ya kuanza kutumika rasmi. Basi hilo lina kamera zenye uwezo wa kuhisi wa hali ya juu, rada ya ultrasonic, rada ya leza na vifaa vingine vya kuhisi, ambavyo kwa pamoja vinaunda "macho" ya basi hilo. Magari hayo yanaweza kutambua taa za kuongoza watumiaji wa barabara, alama za barabarani na mistari ya njia za barabarani n.k., na kufanya vitendo vya kufuata kwa nyuma magari mengine, kuyapita magari mengine na kujiegesha.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha