Zambia yazindua kiwanda cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 17, 2023
Zambia yazindua kiwanda cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua
Wafanyakazi wakishiriki kwenye hafla ya kuunganishwa kwa gridi ya umeme ya taifa katika kiwanda cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua huko Kitwe, Zambia, Februari 15, 2023. (Xinhua/Martin Mbangweta)

KITWE - Zambia siku ya Jumatano imezindua kiwanda cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uwezo wa kuzalisha umeme wa nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika.

Kiwanda cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua cha Riverside katika mji wa Kitwe, Mkoa wa Copperbelt ni mradi wa Shirika la Nishati la Copperbelt, kampuni iliyoorodheshwa kwenye soko la hisa ambayo hutoa huduma ya umeme kwa sekta ya madini nchini humo.

Kampuni hiyo, ambayo awali ilizindua mradi wake wenye kuzalisha umeme wa nguvu za Megawati 1 Mwaka 2018, ilitia saini makubaliano na kampuni ya ujenzi ya China ya Sinohydro kwa ajili ya uhandisi na ujenzi mnamo Novemba 2021 ili kuongeza uwezo wa kiwanda hicho cha kuzalisha umeme unaofikia hadi nguvu za Megawati 34 na uzalishaji wa kila mwaka la nishati yenye nguvu ya 56.5 GWh.

Mradi huo umehusisha uwekaji wa paneli zaidi ya 61,320 za kusharabu miale ya jua na ujenzi wa njia mbili za kusambaza umeme. Jumla ya dola milioni 22 za Marekani zimewekezwa katika mradi huo wa upanuzi.

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amesema kwenye hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho kwamba uwekezaji huo ni mafanikio makubwa kuelekea lengo la nchi hiyo la kukomesha kukatika kwa umeme, kunakojulikana nchini humo kama upunguzaji wa mzigo. Kwa mujibu wa hotuba yake, serikali inakusudia kuongeza maradufu uwezo wa kuzalisha umeme nchini humo ili kusaidia mahitaji ya viwanda.

Rais wa huyo wa Zambia amesisitiza kuwa usalama wa nishati ni muhimu kwa nchi hiyo kwa sababu unachochea sekta ya viwanda na ameipongeza kampuni hiyo kwa kukamilisha juhudi za serikali za kuimarisha uzalishaji wa umeme hasa kwa kuzalisha nishati safi au ya kijani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha