Ujenzi wa mabamba ya reli kwenye Reli ya Mwendokasi ya Jakarta-Bandung wakamilika (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 16, 2023
Ujenzi wa mabamba ya reli kwenye Reli ya Mwendokasi ya Jakarta-Bandung wakamilika
Picha hii iliyopigwa Februari 15, 2023 ikionyesha eneo la ujenzi wa mabamba ya mwisho ya Reli ya Mwendokasi ya Jakarta-Bandung huko Karawang, Java Magharibi, Indonesia. (Xinhua/Xu Qin)

JAKARTA- Huku zege likimiminwa kwenye bamba la mwisho siku ya Jumatano, ujenzi wa mabamba ya reli kwenye Reli ya Mwendokasi ya Jakarta-Bandung umekamilika.

Urefu wa jumla wa sehemu ya mabamba hayo ni Kilomita 85.3, ikiwa ni asilimia 60 ya reli nzima, ambayo ina urefu wa Kilomita 142.3. Kwa jumla mabamba 30,177 yanatakiwa kuwekwa.

Matumizi ya CRTS III ya mabamba yanatokana na teknolojia ya China yenye hakimiliki ya ubunifu. Aina hii mpya ya mabamba ya reli ina faida za muundo rahisi, ufanisi thabiti na uimara mzuri, na ni rahisi kuunda. Ni moja ya teknolojia muhimu kuhakikisha ulaini na usalama wa reli ya mwendo kasi.

Kwa sasa, kazi zote za ujenzi wa daraja dogo, daraja na kituo zimekamilika. Reli hiyo imepangwa kuanza kufanya kazi katikati ya mwaka huu.

Njia hiyo ya reli ya mwendo kasi, ambayo ni mradi wa kihistoria chini ya Mpango wa Ukanda Mmoja, Njia Moja unaopendekezwa na China, inaunganisha mji mkuu wa Indonesia, Jakarta na mji mwingine mkubwa wa Bandung.

Ikiwa na kasi ya kilomita 350 kwa saa, reli hiyo itapunguza umbali wa safari kati ya Jakarta na Bandung kutoka zaidi ya saa tatu hadi dakika 40 hivi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha