

Lugha Nyingine
Meli mbili za usafirishaji zilizoundwa na China zatoka kwenye Gati huko Shanghai (2)
![]() |
Meli ya kusafirisha Gesi Asilia Kimiminika ya Mark III yenye uwezo wa mita za ujazo 79,800 ikitoka kwenye gati Tarehe 15, Februari,. (Picha/Liang Jing) |
Tarehe 15, Februari, meli mbili za usafirishaji za kwanza kuundwa nchini China zilitoka kwenye Gati No.4 la Kampuni ya Uundaji Meli ya Jiangnan, ambayo inamilikiwa na Shirika la Kuunda Meli la China. Meli hizo mbili za kwanza ni Meli ya Mark III ya kusafirishia Gesi Asilia ya Kimiminika (LNG) yenye uwezo wa mita za ujazo 79,800, na Meli Kubwa ya kusafirishia Gesi Asilia ya Kimiminika yenye uwezo wa mita za ujazo 93,000 (VLGC).
Kati ya meli hizo mbili, meli ya LNG yenye uwezo wa mita za ujazo 79,800 imeundwa kikamilifu kwa kujitegemea na kampuni ya Uundaji Meli ya Jiangnan. Meli hii ina muundo wa urefu wa mita 229.99, upana wa mita 36 na kimo cha mita 21.5. Ilianza kuundwa Desemba, 2021, na kutia nanga kwenye gati Agosti, 2022.
Meli hiyo ya LNG ni meli ya kwanza ya Mark III ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma