

Lugha Nyingine
Roketi ya kibiashara ya China CERES-1 Y5 yarusha satelaiti 5 kwenye anga ya juu (2)
![]() |
Roketi ya kubeba mizigo ya CERES-1 Y5 ikiruka kutoka Kituo cha Urushaji Satellite cha Jiuquan, Kaskazini-Magharibi mwa China, Januari 9, 2023. (Picha na Wang Jiangbo/Xinhua) |
JIUQUAN - China Jumatatu ilirusha roketi ya kubeba ya CERES-1 Y5 kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini Magharibi mwa China.
Roketi hiyo ya kibiashara iliruka majira ya saa 7:04 Mchana (Saa za Beijing) kutoka kwenye eneo la urushaji, ikituma satelaiti tano kwenye obiti iliyopangwa.
Satelaiti hizo tano ni pamoja na satelaiti ya Tianqi-13 itakayokuwa kwenye kundinyota la Tianqi, satelaiti mbili za kundinyota la hali ya hewa la Tianmu-1, na nyingine mbili za ufuatiliaji wa Dunia na uenezaji wa sayansi ya anga, mtawalia.
Ikiwa imeundwa na kampuni ya teknolojia ya juu ya Beijing ya Galactic Energy, Roketi ya CERES-1 ni roketi ndogo ya kubeba yenye uwezo wa kutuma satelaiti ndogo kwenye obiti.
Urushaji huo ulikuwa safari ya tano ya vyombo vya anga ya juu kwa mfululizo wa roketi za CERES-1.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma