

Lugha Nyingine
Cyprus na India zasaini Makubaliano ya Maelewano juu ya ushirikiano wa ulinzi
NICOSIA - Cyprus na India Alhamisi zimetia saini Makubaliano ya Maelewano (MoU) kuhusu ulinzi na ushirikiano wa kijeshi na zimesisitiza kuimarisha uhusiano wao wa karibu kwa zaidi ya miaka 60, nchi hizo mbili zimesema katika taarifa rasmi.
Makubaliano hayo yametiwa saini wakati wa ziara ya kikazi nchini Cyprus ya Waziri wa Mambo ya Nje wa India Subrahmanyam Jaishankar.
Taarifa hiyo imesema kuwa Jaishankar na mwenzake wa Cyprus, Ioannis Kasoulides, pia wametia saini Makubaliano ya Kujiunga kwa Cyprus kwenye Jumuiya ya Kimatifa ya Nishati ya Jua (ISA).
ISA inalenga kuhimiza ushirikiano katika uzalishaji na matumizi bora ya nishati ya jua ili kupunguza utegemezi wa nishati ya mafuta.
Akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Cyprus Nicos Nouris, Jaishankar pia alitia saini Barua ya Nia ya kuanzisha mazungumzo ya makubaliano ya uhamiaji na matembezi ya watu kwa lengo la kudhibiti uhamiaji usio wa kawaida.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma