

Lugha Nyingine
Timu ya 39 ya China ya utafiti wa Ncha ya Kusini ya Dunia yafunga safari
Watafiti wa kwanza wa Timu ya 39 ya China ya utafiti wa Ncha ya Kusini ya Dunia walipanda meli ya Xuelong No.2 ya utafiti wa Ncha ya Kusini ya Dunia wakafunga safari kutoka kwenye bandari ya kituo cha utafiti wa ncha ya dunia cha China iliyopo Shanghai, China, ili kwenda eneo la Ncha ya Kusini ya Dunia kutekeleza jukumu la utafiti wa kisayansi.
Habari zilisema, kwa jumla wapo watafiti 255 kwenye Timu ya 39 ya China ya utafiti wa kisayansi wa ncha ya kusini ya dunia, ambao wataondoka kwa vikundi viwili. Hii ni mara ya tatu kwa China kutafiti eneo la ncha ya dunia kwa kupanda meli mbili za Xuelong. Timu hiyo ya watafiti inatarajiwa kurudi China mwanzoni mwa mwezi Aprili, mwaka 2023.
Utafiti wa kisayansi wa China wa mara 39 kwenye eneo la ncha ya kusini ya dunia utalenga namna ya kuitika mabadiliko ya tabianchi ya dunia na masuala mengi muhimu ya kisayansi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma