

Lugha Nyingine
Wanaanga wa China watoa mafunzo katika kituo cha anga ya juu cha China (2)
Mafunzo ya tatu yalitangazwa moja kwa moja kutoka kwenye Kituo cha anga ya juu cha China mchana wa Jumatano ya wiki hii, ambapo wanaanga walioko kwenye chombo cha anga ya juu cha Shanzhou-14 Chen Dong, Liu Yang na Cai Xuzhe walitoa mafunzo hayo kwa wanafunzi waliopo kwenye ardhi ya dunia.
Darasa kuu la wanafunzi lilikuwapo kwenye Kituo cha teknolojia na uhandisi wa matumizi ya nafasi za anga ya juu katika Taasisi kuu ya Sayansi ya China. Wanafunzi wengine wanasikiliza mafunzo kwenye madarasa mengine matatu ya mikoa ya Yunnan, Henan na Shandong ya China.
Huu ni mjadala wa kwanza wa sayansi kuhusu moduli ya maabara ya Wentian kwenye anga ya juu. Mafunzo ya kwanza na pili ya “Darasa la Tiangong” yalitolewa na wanaanga waliokuwepo kwenye chombo cha Tianhe katika chombo cha anga ya juu cha Shanzhou-13, ambacho ni chombo cha kiini cha Kituo cha anga ya juu cha China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma