

Lugha Nyingine
Ndege ya zimamoto AG600M “Kunlong” yamaliza majaribio ya kuvuta na kumwaga maji
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 28, 2022
![]() |
Ndege ya zimamoto ya AG600M ikiruka kutoka kwenye uso wa maji katika majaribio ya kuvuta na kumwaga maji huko Jingmen, Mkoa wa Hubei wa China, Septemba 27, 2022. (Xinhua/Wu Zhizun) |
Ndege ya zimamoto ya AG600M “Kunlong”, ambayo ilisanifiwa na kutengenezwa na China yenyewe, ilifaulu kumaliza majaribio ya kuvuta na kumwaga maji tani 12 kwenye uwanja wa ndege wa Zhanghe, Mji wa Jingmen wa Mkoa wa Hubei wa China, Tarehe 27, Septemba. Matarajio hayo kwa uwezo wa ndege ya AG600M wa kuvuta na kumwaga maji ni jambo lingine lenye umuhimu mkubwa baada ya urukaji wake wa kwanza kutoka ardhi tarehe 31, Mei na urukaji wake wa kwanza kutoka kwenye uso wa maji tarehe 29, Agosti. Ndege ya AG600 ni chombo muhimu kinachotengenezwa na China kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya kujenga mfumo wa uokoaji wa dharura na mfumo wa kitaifa wa kuzuia maafa na kufanya uokozi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma