

Lugha Nyingine
China yarusha satelaiti ya Zhongxing-1E kwenye anga ya juu
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 14, 2022
WENCHANG, Hainan - China siku ya Jumanne imefanikiwa kutuma setilaiti mpya kwenye anga ya juu kutoka kwenye Eneo la Kurusha vyombo kwenda anga ya juu la Wenchang katika Mkoa wa Kisiwa wa Hainan ulioko Kusini mwa nchi hiyo.
Satelaiti hiyo, Zhongxing-1E, imerushwa saa 9:18 alasiri. (Saa za Beijing) kwa kutumia roketi iliyoboreshwa ya Long March-7 na kuingia kwenye obiti iliyopangwa kwa mafanikio. Satelaiti hiyo itatoa huduma za kiwango cha juu za sauti, data, redio na televisheni.
Hii ni misheni ya 437 kwenye anga ya juu kwa roketi za kubeba za safu ya Long March.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma