China yafanya mkutano kuhusu ustaarabu wa mtandao wa intaneti

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 29, 2022
China yafanya mkutano kuhusu ustaarabu wa mtandao wa intaneti
Mtembeleaji akipata uzoefu wa matumizi ya vifaa vya uhalisia pepe (VR) kwenye maonesho ya Mkutano wa Ustaarabu wa Mtandao wa Intaneti wa China Mwaka 2022 huko Tianjin, Kaskazini mwa China, Agosti 28, 2022. Mkutano wa siku mbili wa Ustaarabu wa Mtandao wa Intaneti wa China kwa Mwaka 2022 unajumuisha jukwaa kuu, jukwaa la kuhimiza uadilifu katika anga ya mtandao wa intaneti, majukwaa madogo 10, maonyesho na shughuli moja yenye mada mahsusi. (Xinhua/Sun Fanyue)

TIANJIN- Mkutano wa kuhimiza ustaarabu wa mtandao wa intaneti umefunguliwa Jumapili alasiri katika Manispaa ya Tianjin, Kaskazini mwa China.

Mkutano huo wa siku mbili wa Ustaarabu wa Mtandao wa Intaneti wa China Mwaka 2022 unajumuisha jukwaa kuu, jukwaa la kuhimiza uadilifu katika anga ya mtandao wa intaneti, majukwa madogo 10, maonyesho na shughuli moja yenye mada mahsusi.

Tangazo la kuhimiza ustaarabu wa mtandao wa intaneti kwa pamoja limetolewa, likiwa na makubaliano ya vipengele sita juu ya kuimarisha ujenzi wa ustaarabu wa mtandao wa intaneti katika zama mpya katika maeneo kama vile ikolojia ya mtandao, utamaduni na usalama.

Maonyesho ya mkutano huo, yanafanyika mtandaoni na nje ya mtandao, yamefunguliwa ili kuangazia maendeleo ambayo China imepata katika kuhimiza ustaarabu wa mtandao tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ulipofanyika Mwaka 2012.

Kwa upande wa makongamano madogo yanajihusisha na mada mbalimbali kuanzia ukuzaji wa maudhui, ikolojia na utawala unaozingatia sheria kwenye nafasi za mtandao wa intaneti hadi usimamizi wa kanuni, mabadilishano ya kimataifa na ulinzi wa faragha kwenye mtandao wa intaneti. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha