

Lugha Nyingine
Maonesho ya Teknolojia za Akili Bandia ya China yafunguliwa huko Chongqing (2)
Maonesho ya teknolojia za akili bandia ya China 2022 Jumatatu yalifunguliwa huko Chongqing, Kusini Magharibi mwa China, yakivutia washiriki zaidi ya 500 kutoka ndani na nje ya China kuja kuonesha matunda yao mapya zaidi ya teknolojia za akili bandia.
Maonesho hayo ya siku tatu yakiwa na kaulimbiu ya "teknolojia za akili bandia: kuwezesha uchumi, kustawisha maisha", yatahusisha makongamano 20, shughuli zaidi ya 120 za kutangaza bidhaa na teknolojia mpya, na mashindano zaidi ya 10 na shughuli nyingine kadha wa kadha.
Maonesho hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka mjini Chongqing kuanzia Mwaka 2018, yakiwa ni jukwaa muhimu la kuhimiza mawasiliano ya teknolojia za akili bandia duniani na ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya viwanda vinavyotumia akili bandia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma