

Lugha Nyingine
Maonesho ya Mkutano wa Kimataifa wa Roboti (WRC) katika Mji wa Beijing yaonyesha teknolojia na bidhaa mpya za roboti (9)
![]() |
Msichana akitazama roboti ya upasuaji kwenye Maonesho ya Mkutano wa Kimataifa wa Roboti (WRC) 2022 wa Beijing, Agosti 19, 2022. (Xinhua/Ju Huanzong) |
BEIJING - Zaidi ya seti 500 za roboti kutoka makampuni 130 zilionyeshwa kwenye Maonesho ya Mkutano wa Kimataifa wa Roboti (WRC) 2022 katika Mji wa Beijing, kati ya roboti hizo, zaidi ya 30 zilionyeshwa kwa mara ya kwanza duniani.
Mkutano huo wa roboti, uliofanyika kuanzia Agosti 18 hadi 21, ulijumuisha kongamano, maonyesho na mashindano ya roboti.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wataalam zaidi ya 300 kutoka nchi na maeneo 15 duniani, ambapo walinufaika pamoja na mafanikio ya teknolojia ya kisasa ya kitaaluma na mwelekeo wa maendeleo katika sekta ya robotiki, kama vile roboti za teknolojia ya hali ya juu na otomatiki, akili bandia (AI), kujifunza kwa kutumia mashine, utengenezaji wa bidhaa kwa kutumia akili bandia, kiolesura cha kompyuta ya ubongo (BCI) na mwingiliano wa akili bandia kati ya mashine na binadamu.
Kwa upande wa mashindano ya roboti, yalihusisha maeneo manne muhimu ambayo ni, mashindano ya roboti ya Tri-Co, Mashindano ya BCI yanayoendeshwa na Roboti, mashindano ya matumizi ya roboti, na mashindano ya uvumbuzi kwa vijana, na yalivutia washiriki wapatao 4,000 ambao wakishindana kwenye uwanja huo.
Mkutano wa Kimataifa Roboti umekuwa ukifanyika Beijing kwa mara sita mfululizo tangu Mwaka 2015.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma