China yaanza kusafirisha treni za mwendo kasi kwenda Indonesia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 22, 2022
China yaanza kusafirisha treni za mwendo kasi kwenda Indonesia
Picha iliyopigwa Agosti 18, 2022 kutoka angani ikionyesha treni ya abiria ya mwendo kasi, iliyoundwa mahususi kwa ajili ya reli ya mwendo kasi ya Jakarta-Bandung, ikipakiwa kwenye meli katika Bandari ya Qingdao, Mkoa wa Shandong nchini China. Seti ya treni za abiria na treni ya ukaguzi zimesafirishwa hadi Indonesia, ikiwa ni kuashiria maendeleo muhimu katika ujenzi wa reli hiyo, ambayo ni mradi wa kihistoria chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja. (Picha na Jiang Chao/Xinhua)

QINGDAO - Treni ya abiria ya mwendo kasi na treni ya ukaguzi, iliyoundwa mahususi kwa ajili ya reli ya mwendo kasi ya Jakarta-Bandung nchini Indonesia, iliondoka kwenye Bandari ya Qingdao katika Mkoa wa Shandong, nchini China siku ya Jumapili.

Treni hizo zimeundwa na kutengenezwa na Kampuni ya CRRC Qingdao Sifang kwa ajili ya mradi wa kihistoria chini ya Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, treni za kwanza zitawasili Jakarta, Indonesia mwishoni mwa Agosti, na treni zilizosalia uwasilishaji wake utakamilika hadi ifikapo mwanzoni mwa Mwaka 2023.

Treni hizo zikiwa zimeundwa kwa teknolojia ya hali ya juu ya treni ya mwendo kasi ya Fuxing, zina mwendo kasi wa kilomita 350 kwa saa na zimeundwa na kutengenezwa kuendana na viwango vya teknolojia ya China, na kuweza kuhimili mazingira ya usafirishaji na hali halisi ya laini nchini Indonesia, na vile vile utamaduni wa nchini humo.

Ikiwa na jumla ya urefu wa kilomita 142, reli hiyo ya mwendo kasi ya Jakarta-Bandung inaunganisha Jakarta, Mji Mkuu wa Indonesia, na Bandung, ambao ni mji maarufu wa kitalii nchini Indonesia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha