

Lugha Nyingine
Wanaanga wa China kwenye Chombo cha Shenzhou No.14 waingia kwenye moduli ya msingi ya kituo cha anga ya juu (5)
![]() |
Picha iliyopigwa Juni 5, 2022 kwenye skrini katika Kituo cha Udhibiti wa Usafiri Kwenye Anga ya Juu cha Beijing ikiwaonesha wanaanga watatu wa China wakiingia kwenye moduli ya msingi ya kituo cha anga za juu cha Tianhe. (Xinhua/Li Xin) |
BEIJING - Idara ya Usafiri Kwenye Anga ya Juu ya China (CMSA) imesema kuwa, wanaanga watatu wa China waliokuwa kwenye chombo cha anga za juu cha Shenzhou No.14 jana Jumapili waliingia kwenye moduli ya msingi ya kituo cha anga za juu cha Tianhe.
Baada ya Shenzhou No.14 kukamilisha kwa ufanisi mzunguko wa otomatiki na kuwezesha kutua kwa pamoja kwenye moduli ya Tianhe, chombo cha kubeba mizigo cha Tianzhou No. 3 na chombo cha kubeba mizigo cha Tianzhou No.4, wanaanga wa Shenzhou No.14 waliingia kwenye kifaa cha obiti kutoka kwenye kifaa cha kurejea ardhini cha chombo cha anga za juu.
Baada ya mfululizo wa maandalizi, mmoja wa wanaanga hao Chen Dong alifungua sehemu ya moduli ya msingi ya Tianhe. Hadi kufikia saa 8:50 mchana (kwa saa za Beijing), wanaanga Chen Dong, Liu Yang na Cai Xuzhe walikuwa wameingia kwenye chombo cha Tianhe mmoja baada ya mwingine.
Kwa muujibu wa CMSA, wanaanga hao watatu watafanya kazi husika zilizopangwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma