

Lugha Nyingine
Rais Xi akutana na mashujaa, watu wa mifano ya kuigwa kutoka idara za usalama wa umma (2)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping jana Jumatano alikutana na wajumbe wa mkutano wa kuwapongeza mashujaa na watu wa mifano ya kuigwa kutoka idara za usalama wa umma.
Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, ametoa pongezi nyingi kwa wajumbe hao, na kutoa salamu za dhati kwa polisi na maofisa wa polisi, pamoja na polisi wasaidizi kutoka kote nchini China.
Li Keqiang na Wang Huning, ambao wote ni wajumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, walihudhuria kwenye mkutano huo.
Xi alikuwa na mazungumzo ya dhati na alipiga picha na wajumbe hao katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.
Guo Shengkun, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Mkuu wa Kamati ya Siasa na Sheria ya Kamati Kuu ya CPC, alitoa hotuba katika mkutano huo.
Ametoa wito kwa idara za usalama wa umma kote nchini China kutekeleza kwa kina Fikra ya Xi Jinping kuhusu Utawala wa kisheria, na kukidhi matakwa ya kuwa waaminifu kwa CPC, kuwatumikia wananchi, kutokuwa na upendeleo katika utekelezaji wa sheria na kufuata nidhamu kali kwa umakini.
“Juhudi madhubuti zinapaswa kufanywa ili kuzuia hatari, kuhakikisha usalama na kudumisha utulivu” Guo amesisitiza.
Jumla ya vikundi 982 na watu 1,485 kutoka idara za usalama wa umma walipongezwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma