Chombo cha Kurudi kwenye ardhi ya dunia cha Shenzhou No. 13 chafunguliwa Beijing (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 27, 2022
Chombo cha Kurudi kwenye ardhi ya dunia cha Shenzhou No. 13 chafunguliwa Beijing
(Picha inatoka Chinanews.)

Katika mchana wa Tarehe 26, Aprili, chombo cha kurudi kwenye ardhi ya dunia cha chombo cha kubeba binadamu kwenye anga ya juu Shenzhou No. 13 kilifunguliwa hapa Beijing. Kutoka kwenye chombo hicho, vitu vingi vimetolewa, vikiwemo mbegu za mazao za mimea za Serikali za Mkoa wa Yunnan, Mkoa unaojiendesha wa Wahui wa Ningxia, Mji wa Yuzhou wa Mkoa wa Shaanxi, Chuo Kikuu cha Kilimo cha China, Chuo Kikuu cha Misitu cha China, Taasisi ya Sayansi ya Kilimo na Misitu ya Beijing, Kampuni ya Mbegu ya Zhongnongfa na Shirikisho la uvumbuzi la viwanda vya kuotesha mbegu kwenye anga ya juu, kadi ya Kituo Kikuu cha Radio na Televishen cha China kuhusu hifadhi ya video na picha bora zilizopigwa na wanaanga kwenye obiti, stempu za kumbukumbu za Tawi la Beijing la Kampuni ya Posta ya China, pamoja na picha zilizochorwa na vijana na watoto wa Hong Kong kutoka Taasisi ya Tano ya Kundi la Teknolojia ya Safari kwenye anga ya juu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha