Kituo cha kuzalisha Umeme kwa nishati ya Maji cha Baihetan chafanya juhudi kuanza uzalishaji (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 25, 2022
Kituo cha kuzalisha Umeme kwa nishati ya Maji cha Baihetan chafanya juhudi kuanza uzalishaji
Picha iliyopigwa Aprili 22 ikionesha muonekano wa Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa nishati ya Maji cha Baihetan. (Picha na droni)

Kwa sasa, kazi za mwisho za kuunganisha seti mbili za genereta za Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa nishati ya Maji cha Baihetan zimekaribia kumalizika, na mradi huo umeingia katika kipindi cha mwisho cha kuanza kuzinduliwa kikamilifu.

Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa nishati ya Maji cha Baihetan kiko kwenye sehemu kuu ya Mto Jinsha ambayo iko kwenye makutano ya mpaka wa Wilaya ya Ningnan ya Mkoa wa Sichuan na Wilaya ya Qiaojia ya Mkoa wa Yunnan. Ni mradi mkubwa wa kitaifa wa kutekeleza "Usambazaji wa Umeme kutoka Magharibi hadi Mashariki". Jumla ya uwezo wa uzalishaji ni kilowatisaa milioni 16. (Mpiga picha: Hu Chao)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha