Ukraine na Russia zakubaliana kuhamisha wanawake, watoto na wazee kutoka Mariupol (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 21, 2022
Ukraine na Russia zakubaliana kuhamisha wanawake, watoto na wazee kutoka Mariupol
Mkazi akipita majengo yaliyoharibiwa huko Mariupol, Aprili 19, 2022.

Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk Jumatano alisema, Ukraine na Russia zimekubaliana kwa hatua ya mwanzo kuanzisha ukanda wa kibinadamu kwa ajili ya kuwahamisha wanawake, watoto na wazee kutoka Mariupol, ambao unashambuliwa kwa vita.

Vereshchuk aliandika kwenye Telegram kuwa, wakazi wa Mariupol watahamishiwa Zaporizhzhia, mji wa Kusini mwa Ukraine, kwa kupitia Wilaya ya Berdyansk, inayodhibitiwa na vikosi vya jeshi la Russia.

Wakati huohuo, meya wa mji wa Mariupol Vadym Boichenko alisema kupitia televisheni ya taifa kuwa, Ukraine inatumai kupeleka mabasi 90 kwenye mji huo uliozingirwa ili kuwahamisha wanawake, watoto na wazeze 6,000 hivi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha