Roketi ya Yao E ya Changzheng No.7 yawasilishwa salama kwenye uwanja wa kurusha satelaiti wa Wenchang (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 12, 2022
Roketi ya Yao E ya Changzheng No.7 yawasilishwa salama kwenye uwanja wa kurusha satelaiti wa Wenchang
Roketi ya Yao E ya Changzheng No.7 iko kwenye njia ya kuwasilishwa. (Mpiga picha:Du Xinxin)

Waandishi wa habari walipata habari kutoka kwa Ofisi ya mradi wa China wa kupeleka chombo kinachobeba binadamu kwenye safari ya anga ya juu kuwa, roketi ya Yao E ya Changzheng No.7 ambayo itapeleka chombo cha kubeba mzigo Tianzhou No.4 kwenye anga ya juu imekamilishwa kazi zote za utafiti na utengenezaji, na kuwasilishwa salama kwenye uwanja wa kurusha satelaiti wa Wenchang Aprili 11.

Baadaye, Roketi ya Yao E ya Changzheng No.7 na chombo cha kubeba mzigo kwenye safari ya anga ya juu cha Tianzhou No.4 ambacho kimewasilishwa mapema vitaanza kufanyiwa kazi ya kufungwa na kufanyiwa majaribio kwa mpango uliowekwa kwenye eneo la uwanja wa kurusha satelaiti.

Hivi sasa, hali ya vifaa vya uwanja wa kurusha satelaiti inaonekana ni nzuri, mifumo mbalimbali ya kufanyiwa majaribio inafanya maandalizi mbalimbali ya majukumu kwa utaratibu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha