

Lugha Nyingine
China yarusha satelaiti mpya ya ufuatiliaji wa dunia (3)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 07, 2022
![]() |
Roketi za Changzheng 4C zilizobeba satelaiti Gaofen-3 03 zikiruka kutoka Kituo cha Kurusha Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini Magharibi mwa China, Aprili 7, 2022. (Xinhua) |
Leo Alhamisi China imerusha satelaiti mpya ya ufuatiliaji wa dunia kutoka Kituo cha Kurusha Satelaiti cha Jiuquan kilichoko Kaskazini Magharibi mwa China.
Satelaiti hiyo, Gaofen-3 03, ilirushwa kwa kutumia roketi za Changzheng 4C saa moja dakika 47 asubuhi (kwa saa za Beijing) na imefaulu kuingia kwenye obiti iliyopangwa.
Kazi hiyo ya kurusha satelaiti ni safari ya 414 ya roketi za aina ya Changzheng.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma