

Lugha Nyingine
Kituo cha Anga ya Juu cha China chafanikisha kutoa mafunzo kutoka anga ya juu kwa mara ya pili (4)
Mchana wa Tarehe 23, Machi, mafunzo ya pili ya “Darasa la Tiangong” yalianza rasmi huku yakitangazwa moja kwa moja kupitia mtandao wa intaneti kwenye kituo cha anga ya juu cha China. Wanaanga watatu wa Shenzhou No.13 Zhai Zhigang, Wang Yaping, Ye Guangfu walitoa mafunzo hayo. Hii ni mara ya pili kwa kituo hiki cha China kutoa mafunzo kwenye anga ya juu, na pia ni mara ya tatu kwa wanaanga wa China kutoa mafunzo kutoka anga ya juu.
Wakati wa mafunzo hayo yaliyochukua dakika 45 hivi, wanaanga hao walishirikiana, wakionesha kwa udhahiri majaribio mbalimbali ya kiteknolojia katika mazingira yenye nguvu kidogo ya mvutano, kueleza kanuni za kisayansi za majaribio hayo, kuonesha baadhi ya vifaa vya kisayansi kwenye anga ya juu, na kujulisha mazingira ya kazi na maisha yao katika kituo hicho. Wakati wa muhadhara, wanaanga walifanya maingiliano na walimu na wanafunzi walioko duniani kwa kupitia video.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma