Mradi wa Televisheni za Satelaiti Vijijini Wawasaidia Wanavijiji wa Rwanda kutazama Michezo ya Olimpiki (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 07, 2022
Mradi wa Televisheni za Satelaiti Vijijini Wawasaidia Wanavijiji wa Rwanda kutazama Michezo ya Olimpiki
Februari 4, katika kijiji kimoja kilichoko kwenye kitongoji cha Kigali, Wanakijiji wakitazama Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing. (Picha/Xinhua)

Wakati wa kipindi cha kufunguliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, watekelezaji wa Mradi wa “kuunganisha vijiji elfu 10 na televisheni” nchini Rwanda, ambao ni wahandisi wa Kampuni ya StarTimes ya China wanajitahidi zaidi kufanya kazi ya kila siku ya kukagua na kutengeneza zana na vifaa, ili kuhakikisha watumiaji wanaweza kutazama michezo hiyo kwenye televisheni. Mradi huo wa “kuunganisha vijiji elfu 10 na televisheni” ambao ni msaada wa China kwa Afrika, nchini Rwanda ulikamilika Mei, 2019. Umetoa fursa ya kufunga televisheni za kidijitali za satelaiti kwa vijiji 300, sehemu 900 za umma na familia 6000 nchini Rwanda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha