Timu ya Wanasayansi yafanya Utafiti wa kisayansi kwenye Barafu Katika Mlima Amne Machin

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 11, 2022
Timu ya Wanasayansi yafanya Utafiti wa kisayansi kwenye Barafu Katika Mlima Amne Machin
(Picha inatoka CFP.)

Hivi karibuni, Timu ya wanasayansi kutoka Kamati ya Uhifadhi wa Maji ya Mto Changjiang imefanya utafiti wa kisayansi kwenye barafu kwa siku tatu kwenye Mlima Amne Machin, ambao uko kwenye eneo la chanzo cha Mto Manjano la Bustani ya Taifa ya Sanjiangyuan.

Kilele kirefu zaidi cha Mlima Amne Machen kina urefu wa mita 6282 kutoka usawa wa bahari, kikifunikwa na theluji isiyoyeyuka mwaka mzima kwenye chanzo cha Mto Manjano.

Wataalam wamefahamisha kuwa, mto wa barafu wa Weigele Dangxiong wa Mlima Amne Machen ni hifadhi kubwa ya maliasili ya maji. Lengo kuu la utafiti huo ni kutumia satelaiti, UAV na njia nyingine za kiteknolojia kujenga mfumo kamilifu wa kufuatilia, na kutathmini kutoka pande zote mabadiliko ya mto wa barafu katika mazingira asilia ya Mto Manjano pamoja na athari inayohusiana na maafa ya kijiolojia na ya hali ya hewa yaliyotokea kwenye eneo la mtiririko wa Mto Manjano.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha