

Lugha Nyingine
Kisukuku cha kiini cha mimba ya Dinosau cha kikamilifu zaidi Duniani Chagunduliwa nchini China
Kisukuku hicho chenye historia ya miaka milioni 72 hadi milioni 66 ni cha kiini cha mimba ya dinosau aina ya theropod asiye na meno, na ni kisukuku cha kiini cha mimba ya dinosau kilicho kikamilifu zaidi kuwahi kurekodiwa kwenye kumbukumbu za kisayansi hadi leo.
Jumatano ya wiki hii Tarehe 22, kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu “Mtoto Yingliang” uliofanyika katika Jumba la Makumbusho ya Sayansi na Teknolojia la Fujian, Profesa Mshiriki Xing Lida kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi ya Jiolojia cha China alisema, kisukuku hicho kiligunduliwa kwenye tabaka la ardhi ya mwishoni mwa zama ya Cretaceous ya Mji wa Ganjiang, Mkoa wa Jiangxi, Kusini mwa China. Hivi sasa kisukuku hicho kinahifadhiwa kwenye Jumba la Makumbusho ya Miamba ya Asili ya Yingliang la Mkoa wa Fujian.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma