Dawa ya kwanza ya China ya kujikinga dhidi ya Virusi vya Korona yaidhinishwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 13, 2021
Dawa ya kwanza ya China ya kujikinga dhidi ya Virusi vya Korona yaidhinishwa
Picha hii inaonesha Profesa Zhang akionesha sampuli za dawa hiyo. (Chinanews/Jia Tianyong)

Mwishoni mwa wiki iliyoisha, Chuo Kikuu cha Beijing na Chuo Kikuu cha Qinghua kupitia mkutano na waandishi wa habari vilitangaza kuwa, dawa ya kwanza yenye ufanisi maalumu ya kupunguza makali ya Virusi vya Korona na kuongeza kingamwili iliyotengenezwa na Kampuni ya Brii Biosciences ya muunganiko wa BRII-196/BRII-198 imeidhinishwa na Serikali ya China kuuzwa sokoni.

Utafiti wa dawa hiyo uliongozwa na Profesa Zhang Linqi kutoka Chuo Kikuu cha Qinghua. Na kukamilika kwa utafiti na majaribio ya dawa hiyo inaonesha kuwa China imepata dawa ya kwanza yenye ufanisi maalum ya kujikinga dhidi ya virusi vya korona, ambayo imethibitishwa kufanya kazi baada ya kuvuka hatua za utafiti na majaribio mbalimbali ya kitabibu. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha