Lugha Nyingine
Ofisa wa Ghana atoa wito wa kuimarisha usalama wa mtandao wa intaneti ili kukabiliana na uhalifu unaoongezeka mtandaoni

Roboti ikioneshwa kwenye mkutano na maonesho ya “Tech in Ghana Accra 2026” jijini Accra, Ghana, Novemba 24, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)
ACCRA - Jake France, Ofisa wa Usalama wa Mtandao wa Intaneti wa Ghana Jumanne wiki hii amewahimiza waendesha uchumi wa kidijitali kuchukua hatua za usalama zenye nguvu ili kulinda rasilimali na fedha zao wakati huu ambapo kuna ukuaji katika sekta ya teknolojia ya nchi hiyo.
Jake France ni ofisa wa vigezo vya teknolojia vya usalama wa mtandaoni katika Mamlaka ya usalama wa mtandao. Alipotoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano na maonesho ya Tech in Ghana Accra 2026 Jumanne wiki hii alisema, usalama wa mtandao lazima upewe kipaumbele cha juu katika mifumo ya kila mtoa huduma za teknolojia, kutokana na kuongezeka kwa uhalifu wa mtandaoni nchini humo.
France alisema, raia na wafanyabiashara wa Ghana wamekuwa wakikabiliwa na athari kwa mambo yao ya fedha kutokana na vitendo vya ulaghai wa mtandaoni na uhalifu vinavyozidi kuongezeka mtandaoni.
Amesema kuwa kesi za uhalifu wa mtandaoni zilizoripotiwa nchini Ghana zilifikia 4,938, zikiambatana na hasara ya kifedha ya takriban Cedi milioni 209 (dola milioni 17.6 hivi za Marekani) kati ya Januari na Septemba 2026; ikilinganishwa na kesi 4,604 katika mwaka mzima wa 2025.
France amesema takwimu halisi zinaweza hata kuwa kubwa zaidi, kwani baadhi ya waathiriwa hawatoi ripoti kuhusu matukio yaliyowaathiri kwa sababu mbalimbali. "Hii inaonesha kuwa upanuzi wa uchumi wetu wa kidijitali lazima uambatane na hatua imara zaidi za usalama."
"Kwa hivyo, ni lazima tuelewe usalama wa mtandao wa intaneti kuwa ni uwekezaji katika kulinda shughuli za kiuchumi na kudumisha imani ya umma." Amesisitiza.
Carl Ashie, ofisa anayeshughulikia teknolojia ya mambo ya fedha katika Benki Kuu ya Ghana, amesema kuwa miamala ya fedha kwa njia ya simu ya nchi hiyo ilifikia cedi trilioni 4.54 mwaka 2025.

Muoneshaji akionesha mradi wake wa teknolojia kwenye mkutano na maonesho ya Tech in Ghana Accra 2026 jijini Accra, Ghana, Novemba 24, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

Urejeshaji ikolojia waleta uoto wa kijani kwenye kando za Mto Changjiang huko Wuhan, China

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma