Kenya yahimiza uwekezaji binafsi kuendesha juhudi za nishati safi barani Afrika

(CRI Online) Novemba 27, 2026

Kenya imetoa wito kwa sekta binafsi kufanya uwekezaji mkubwa zaidi katika sekta ya nishati barani Afrika, ikitaja ushirikiano wa umma na binafsi (PPPs) na hati fungani za miundombinu ya kijani kama vyombo muhimu vya kupanua upatikanaji wa umeme na kuharakisha mpito wa nishati safi barani humo.

Akihutubia Mkutano wa Nishati Endelevu (SEC) wa mwaka 2026 jana Alhamisi katika mji wa Naivasha nchini Kenya, Waziri wa Nishati na Mafuta James Opiyo Wandayi alisema serikali hazipaswi tena kutegemea ufadhili wa umma tu ili kukidhi mahitaji ya nishati yanayoongezeka barani humo. Ameongeza kuwa serikali ya Kenya itaendelea kuwalinda watumiaji kutokana na gharama zisizo na maana, na kwamba jukumu lao ni kupata uwiano sahihi, ili Wakenya waweze kumudu umeme na uwekezaji uwe na manufaa kwa wale wanaoujenga.

Kama jukwaa kuu la nishati safi na endelevu barani Afrika, mkutano wa SEC wa mwaka huu unafanyika chini ya kaulimbiu "Kuimarisha Mapinduzi ya Viwanda vya Kijani Afrika," na kuwaleta pamoja watunga sera wa kikanda, wazalishaji wa nishati, wawekezaji, washirika wa maendeleo, na wafadhili ili kuchunguza sera, teknolojia, na mifumo ya ufadhili inayohitajika ili kuharakisha mpito wa nishati barani Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha