Xi atoa pongezi kwa mkutano wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuwaunga Mkono Watu wa Palestina

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 25, 2026

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma salamu za pongezi kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Jumatatu kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuwaunga Mkono Watu wa Palestina.

Katika salamu zake hizo, Xi amesema kuwa suala la Palestina ni kiini cha suala la Mashariki ya Kati, na hali ya wasiwasi ya hivi sasa ya eneo hilo haipaswi kukwepesha ufuatiliaji wa jumuiya ya kimataifa kwa suala hilo la Palestina.

Xi amesema, ufunguo wa kutatua suala la Palestina ni kushikilia mwelekeo wa utatuzi wa nchi mbili, na kuhimiza kurejeshwa kwa mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel.

Amesisitiza kuwa kazi za utawala wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Yordani na kujenga upya baada ya vita katika Gaza zinapaswa kuendelezwa kwa kufuata kanuni ya "Wapalestina kutawala Palestina," na kupinga vitendo vyovyote vinavyolenga watu wa Palestina vya kukalia ardhi kwa mabavu au kuvamia haki.

“Jumuiya ya kimataifa inapaswa kubadilisha maoni ya pamoja na ahadi zake vya kuunga mkono Palestina kuwa vitendo halisi, kuhimiza usimamishaji vita wa kudumu katika Gaza na kulinda usalama wa raia,” amesema Xi.

Xi amesema kuwa haki itashinda na haipaswi kukosekana, na siku zote China inaunga mkono kwa uthabiti mambo ya haki ya watu wa Palestina katika kurejesha haki zao halali za kitaifa.

Amesema China itaendelea kushirikiana na nchi zote zinazothamini amani, na kulinda haki katika kuhimiza suala la Palestina litatuliwe mapema iwezekanavyo kwa pande zote, kwa haki, kwa kudumu, kwenye msingi wa kufuata sheria za kimataifa na kwa kuzingatia chanzo cha suala pamoja na hali ilivyo ya sasa.

“Juhudi hizo zitasaidia eneo la Mashariki ya Kati kutimiza amani na utulivu wa kudumu na pia kutoa mchango wa kuhimiza hamasa kwa ajili ya amani, utulivu, maendeleo, na ustawi wa Dunia ,” ameongeza Xi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha