Kampuni ya China yatoa taa za barabarani zinazotumia nishati ya jua nchini Malawi

(CRI Online) Novemba 24, 2026

Kampuni ya China Nyasa Connect Global Limited imetoa taa 20 za barabarani zinazotumia nishati ya jua kwa Halmashauri ya Mji wa Lilongwe na kuahidi kujenga kituo cha mabasi katika mji huo ili kuongeza muunganiko mjini humo.

Akizungumza katika sherehe ya makabidhiano, Mwenyekiti wa kampuni hiyo na makamu wa rais wa Chama cha Wafanyabiashara cha Zhejiang nchini Malawi, Wang Hannan, amesema kuwa mchango huo unaonyesha juhudi endelevu za kampuni hiyo kwa maendeleo ya jamii ya huko na kusisitiza uhusiano mkubwa wa pande mbili kati ya China na Malawi.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Lilongwe Clement Stambuli amekaribisha mchango huo, akibainisha kuwa kituo cha mabasi kilichopangwa kujengwa mjini humo kitarahisisha kwa kiasi kikubwa usafiri wa abiria na mizigo ndani ya mji huo na kwenye wilaya zinazozunguka.

Meya wa Lilongwe Peter Alex Banda pia ameipongeza kampuni hiyo, akisema taa za barabarani za nishati ya jua zitaongeza mwanga utakaowezesha watu kuona zaidi wakati wa usiku na kuboresha usalama wa umma. Ametoa wito wa kupanua ushirikiano na wawekezaji wa China ili kuharakisha juhudi za kufanya mji wa Lilongwe uwe wa kisasa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha