Lugha Nyingine
Viongozi wa Afrika watoa wito wa kuwa na uhuru zaidi kwenye afya ya umma
Viongozi wa Afrika Jumatatu waliitisha Mkutano wa 5 wa Kimataifa kuhusu Afya ya Umma barani Afrika huko Addis Ababa, Ethiopia, wakitoa wito wa kujenga uwezo imara ndani ya Afrika na kupunguza utegemezi wa nje ili kufikia lengo lake la mustakabali wa afya ya umma ya kujitegemea.
Mkutano huo ambao utaendelea hadi Ijumaa chini ya kaulimbiu "Usalama na Uhuru wa Afya wa Afrika: Mabadiliko kutoka Utegemezi wa Afya na Udhaifu hadi Umiliki na Ustahimilivu," unawakutanisha wakuu wa nchi na serikali wa Afrika, mawaziri wa afya, wanasayansi na wavumbuzi, pamoja na washirika wa kimataifa kuangalia hatua zilizopigwa kwenye vipaumbele vya afya vya bara hilo, kutambua mapengo yaliyobaki, na kuendeleza suluhu za kivitendo.
Akihutubia mkutano huo, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Mahmoud Ali Youssouf alitoa wito kwa wanachama wa AU, taasisi za kikanda, na washirika wa maendeleo kuchukua hatua za pamoja na endelevu ili kuharakisha utekelezaji wa ajenda ya uhuru wa afya ya Afrika na kuhakikisha kwamba hakuna Mwafrika anayeachwa nyuma.
Naye Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, ambaye pia ni Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika (AU), ametaka kufanyika kwa mabadiliko ya dhati kutoka ahadi za kisiasa hadi kuongeza ufadhili wa ndani katika sekta ya afya, akisisitiza kuwa uhuru wa Afrika katika masuala ya afya unaanzia kwenye uwekezaji wa Waafrika wenyewe.

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China

Shughuli ya Siku ya Meli ya "Xuelong 2" ya China kufunguliwa kwa umma yafanyika Hainan
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma