Maafisa wa Afrika watoa wito wa ustahimilivu imara wa kiuchumi kufuatia mitikisiko ya kimataifa

(CRI Online) Novemba 24, 2026

Maafisa waandamizi wa Afrika wamesema ni muhimu kuimarisha ustahimilivu wa uchumi wa Afrika ili kufikia ukuaji jumuishi na utulivu wa muda mrefu, kufuatia kuwepo kwa mitikisiko mingi ya nje.

Wakizungumza katika Warsha ya kila Mwaka ya Muungano wa Utafiti wa Kiuchumi wa Afrika jana Jumatatu jijini Nairobi, watunga sera na wataalamu walisisitiza umuhimu wa sera za ndani na uingiliaji kati wa kifedha ili kurudisha bara hilo katika mwelekeo endelevu wa ukuaji.

Waziri wa Fedha na Mipango ya Maendeleo wa Lesotho, Adelaide Retselisitsoe Matlanyane, amesema serikali za Afrika zinaendelea na juhudi za kudumisha utulivu wa uchumi wa jumla, kutoa nafasi za ajira, na kufadhili maendeleo licha ya misukosuko inayoongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi na mivutano ya kijiografia.

Gavana wa Benki Kuu ya Kenya, Kamau Thugge, amesema kuwa utafiti unaozingatia ushahidi ni muhimu katika kuandaa sera zinazokuza uthabiti wa uchumi wa jumla na kuharakisha ukuaji kote barani.

Warsha hiyo ya siku tatu, inayoendeshwa chini ya kaulimbiu "Uchumi wa Jumla, Ukuaji wa Uchumi, na Utawala wa Kidemokrasia," imewakutanisha watunga sera wa ngazi za juu, watafiti, na washirika wa maendeleo ili kuchunguza mazingira mapana ya kiuchumi barani humo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha