Warsha ya China-Afrika yafanyika ili kuimarisha zaidi mifumo ya tahadhari ya mapema ya majanga mbalimbali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 24, 2026

Zhang Wei, Naibu Mkuu wa Ujumbe wa China katika Umoja wa Afrika (AU), akizungumza kwenye warsha ya mafunzo ya China na Afrika juu ya mifumo ya tahadhari ya mapema, AI, na mifumo ya taarifa za kijiografia (GIS) ili kuimarisha uhimilivu wa Afrika na kupunguza athari za hali mbaya ya hewa inayohusiana na El Niño ya mwaka 2026/2027 mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, tarehe 23 Novemba 2026. (Xinhua)

ADDIS ABABA - Maafisa kutoka China na Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) wametoa wito wa kuboreshwa kwa ushirikiano wa kisayansi katika uhimilivu wa tabianchi na kupunguza hatari za majanga ili kusaidia nchi za Afrika kujenga mifumo imara zaidi ya tahadhari ya mapema dhidi ya majanga mbalimbali.

Wito huo umetolewa kwenye warsha ya mafunzo ya China na Afrika iliyofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia jana Jumatatu. Warsha hiyo inajikita katika mifumo ya tahadhari ya mapema, AI, na mifumo ya taarifa za kijiografia (GIS) ili kuimarisha uhimilivu wa Afrika na kupunguza athari za hali mbaya ya hewa inayohusiana na El Niño ya mwaka 2026/2027.

Akizungumza kwenye warsha hiyo, Moses Vilakati, Kamishna wa AU anayeshughulikia kilimo, maendeleo ya vijijini, uchumi wa bluu, na mazingira endelevu, amesema kuwa El Niño ya 2026/2027 inazidi kuwa kali, ikitishia watu hadi milioni 50 kwa njaa na kusababisha hali mbaya ya hewa duniani kote.

"Uzoefu wa El Niño unasisitiza umuhimu wa kuimarisha ufuatiliaji wa tabianchi, utabiri wa misimu, na mifumo ya tahadhari ya mapema ya majanga mbalimbali kwa ajili ya kujiandaa vizuri. Kupitia ushirikiano ulioboreshwa wa kisayansi na matumizi ya AI, kupata ufahamu kwa kutumia mashine, data za satalaiti, na teknolojia za GIS, tunaweza kutabiri vyema hatari zinazohusiana na tabianchi, kubaini makundi ya watu walio katika mazingira dhaifu, na kuunga mkono hatua zinazowahi za kujiandaa ili kulinda maisha na njia za kujikimu," amesema Vilakati.

Zhang Wei, Naibu Mkuu wa Ujumbe wa China katika AU, amesema kuna haja ya dharura kwa Afrika kuimarisha zaidi uwezo wake wa kutoa tahadhari za mapema, na kuongeza uwezo wa jumla wa kuzuia, kupunguza athari, na kuokoa katika majanga, akibainisha kuwa ni asilimia takriban 40 tu ya nchi za Afrika ndizo zimeanzisha mifumo ya tahadhari ya mapema ya majanga mbalimbali.

"Kupitia ushirikiano wa kivitendo katika ufuatiliaji wa hali ya hewa na tahadhari za mapema, kukabiliana na dharura, utafiti wa kisayansi na uvumbuzi wa teknolojia, kuchangia teknolojia, na uendelezaji vipaji, China imeunga mkono nchi za Afrika na mataifa mengine katika kuimarisha uwezo wao wa kuzuia na kupunguza athari za majanga, ikisaidia kulinda maisha na mali za watu," Zhang amesema.

Amesema China pia itafanya kazi na washirika wa Afrika kuanzisha maabara 30 za pamoja na kituo cha ushirikiano wa matumizi ya satalaiti ya kuhisi kwa mbali cha Afrika na China, ili kutoa uungaji mkono zaidi kwa juhudi za Afrika za maendeleo ya kijani na endelevu.

Warsha hiyo, imeandaliwa kwa ushirikiano na Kamisheni ya AU, Ujumbe wa China kwa AU, na Muungano wa Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa ya Sayansi kwa Maeneo ya Ukanda Mmoja, Njia Moja, na itaendelea hadi Ijumaa wiki hii.

Moses Vilakati, kamishna wa Umoja wa Afrika (AU) anayeshughulikia kilimo, maendeleo ya vijijini, uchumi wa bluu na mazingira endelevu, akizungumza kwenye warsha ya mafunzo ya China na Afrika juu ya mifumo ya tahadhari ya mapema, AI, na mifumo ya taarifa za kijiografia (GIS) ili kuimarisha uhimilivu wa Afrika na kupunguza athari za hali mbaya ya hewa inayohusiana na El Niño ya mwaka 2026/2027 mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, tarehe 23 Novemba 2026. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha