Lugha Nyingine
Eisenkot asema hakuna tishio la dharura linalohalalisha shambulio dhidi ya Iran kabla ya kuundwa kwa serikali

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu atakayemaliza muda wake wa madaraka akitoa hotubakwenye mkutano wa chama cha Likud katika bunge la Knesset jijini Jerusalem, Novemba 23, 2026. (Picha na Gil Cohen Magen/Xinhua)
JERUSALEM - Kiongozi wa kundi la upinzani la Israel, Gadi Eisenkot, amesema kuwa hivi sasa haoni tishio la moja kwa moja na la dharura ambalo linaweza kuhalalisha hatua ya kijeshi dhidi ya Iran katika wiki zijazo, au kabla ya kuundwa kwa serikali mpya.
Eisenkot amesema katika taarifa iliyotangazwa radioni kuwa, "Tishio kubwa zaidi kutoka Iran ni kilo 440 za uraniamu iliyorutubishwa ambazo bado hazijateketezwa au kuondolewa, na hilo ndilo jambo tunalopaswa kuliwekea mkazo."
Kauli yake hiyo inatolewa wakati mazungumzo ya kuunda serikali yanapoendelea, na vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kwamba Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu atakayeondoka madarakani anamhimiza Rais wa Marekani Donald Trump kuanzisha mara moja shambulio la kijeshi kwa pamoja dhidi ya Iran, na hata anashinikiza Israel kuanzisha shambulio peke yake dhidi ya Iran.
Kwenye ufunguzi wa mkutano wa chama chake cha Likud katika bunge la Knesset, Netanyahu amesema yeyote anayepuuza uzito wa matishio hayo ya dharura ni kutokana na kusudi la kisiasa.
"Tishio ni halisi na lenye uzito," amesema.
Wakati huo huo shirika la habari la serikali ya Israel, Kan News limeripoti kwamba, Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Israel, Avigdor Lieberman ambaye ni mshirika wa Eisenkot katika kundi la upinzani, amesema kwenye mkutano wa chama chake kwamba, kama Netanyahu atatoa amri ya kuanzisha shambulio la Israel peke yake dhidi ya Iran, amri hiyo itakuwa ni amri haramu ya kukiuka sheria waziwazi.

Waziri Mkuu wa Israel atakayeondoka madarakani Benjamin Netanyahu akitoa hotuba kwenye mkutano wa chama cha Likud katika bunge la Knesset jijini Jerusalem, Novemba 23, 2026. (Picha na Gil Cohen Magen/Xinhua)

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China

Shughuli ya Siku ya Meli ya "Xuelong 2" ya China kufunguliwa kwa umma yafanyika Hainan
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma