Lugha Nyingine
Jukwaa la kubadilishana uzoefu na mbinu za kupunguza umaskini kati ya China na Afrika lafanyika

Xue Songyan, katibu mkuu wa Akademia ya Sayansi ya Jamii ya China, akizungumza kwenye jukwaa la ngazi ya juu kuhusu kupunguza umaskini mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Novemba 21, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)
ADDIS ABABA - Jukwaa maalumu la ngazi ya juu limefanyika Jumamosi mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, ili kuzidisha zaidi ushirikiano kati ya China na Afrika juu ya kupunguza umaskini kupitia kubadilishana uzoefu wa kivitendo na mbinu za maendeleo.
Jukwaa hilo lililofanyika chini ya kaulimbiu ya "Kubadilishana Uzoefu na Mbinu za Kivitendo za Kupunguza Umaskini kati ya China na Afrika", liliwakutanisha pamoja wawakilishi kutoka China, Ethiopia, na nchi nyingine za Afrika ili kuchunguza njia mpya za ushirikiano na kubadilishana maarifa ya kitaasisi kati ya China na Afrika kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za kupunguza umaskini duniani.
Wataalamu na wasomi katika jukwaa hilo wametoa wito wa kubadilisha uzoefu wa pamoja wa maendeleo kuwa suluhisho za kivitendo na zinazozingatia hali halisi ya kila nchi husika huku wakiheshimu njia huru ya maendeleo ya kila nchi, wakibainisha kuwa umaskini si hatma na unaweza kukomezwa kupitia hatua mahsusi, mabadiliko yenye tija, na ushirikiano endelevu.
Akihutubia mkutano huo, Xue Songyan, katibu mkuu wa Akademia ya Sayansi ya Jamii ya China (CASS), alibainisha kuwa China imemaliza kampeni kubwa zaidi ya kupunguza umaskini katika historia ya binadamu, ikitimiza lengo la Umoja wa Mataifa la kupunguza umaskini miaka 10 kabla ya muda uliopangwa.
Jukwaa hilo limesisitiza umuhimu wa uoanishaji wa ushirikiano kati ya China na Afrika na mikakati ya maendeleo ya kitaifa na vipaumbele vya nchi husika, likisisitiza kwamba kupunguza umaskini kunahitaji utawala imara, uungaji mkono wa kitaasisi, na ushiriki mkubwa wa raia.
Tefera Derbew, balozi wa zamani wa Ethiopia nchini China, alisema kuwa umaskini ni changamoto yenye nyanja nyingi inayoathiri heshima, utulivu, na uwezo wa maendeleo wa jamii na mataifa.
Akitoa wito wa kuongeza ushirikiano katika uwekezaji wenye tija, uhamishaji wa teknolojia, na ujengaji uwezo wa ndani, Derbew amesisitiza umuhimu wa kuimarisha zaidi ushirikiano kupitia miradi mahsusi ya nchi inayoendana na vipaumbele vya nchi ambayo inatoa ajira na kusaidia watu kuondoa umaskini kabisa.
Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Ethiopia Chen Hai ameeleza umaskini kuwa ni changamoto ya pamoja inayokabili binadamu, na upunguzaji umaskini na maendeleo kuwa ni masuala yanayohusu ustawi wa binadamu wote.

Balozi wa China nchini Ethiopia Chen Hai, akizungumza kwenye jukwaa la ngazi ya juu kuhusu kupunguza umaskini mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Novemba 21, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)

Tefera Derbew, balozi wa zamani wa Ethiopia nchini China, akizungumza kwenye jukwaa la ngazi ya juu kuhusu kupunguza umaskini mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Novemba 21, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China

Shughuli ya Siku ya Meli ya "Xuelong 2" ya China kufunguliwa kwa umma yafanyika Hainan
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma