Lugha Nyingine
Mashindano makubwa zaidi ya mbio za barabarani barani Afrika yavutia washiriki 60,000 nchini Ethiopia
Mashindano ya "Great Ethiopian Run," mbio kubwa zaidi za barabarani barani Afrika, yalivutia washiriki 60,000 katika barabara za Addis Ababa siku ya Jumapili, ambapo Yismaw Dillu na Yenewa Nibret waliipatia ushindi Ethiopia katika nafasi za ubingwa kwa wanaume na wanawake.
Mbio hizo za kilomita 10, zilizofanyika chini ya kaulimbiu "Mbio Zangu, Rangi Yangu," ziliwakutanisha wanariadha mahiri kutoka Ethiopia na nje ya nchi, pamoja na wakimbiaji wa kujiburudisha wa rika zote, maafisa waandamizi wa Ethiopia, na wanadiplomasia. Dillu alishinda mbio za wanaume kwa mwaka wa pili mfululizo, na Nibret ametwaa taji la wanawake.
Waziri wa Utalii wa Ethiopia, Selamawit Kassa, ambaye alishiriki katika mbio hizo, alisema kuwa tukio hilo lilisaidia kukuza utalii wa michezo na kuitangaza nchi hiyo kimataifa.
Zikiwa zimezinduliwa mwaka 2001, mbio za 'Great Ethiopian Run' zilianzia kutoka mbio za ndani hadi kuwa tukio linalovutia makumi ya maelfu ya washiriki kila mwaka, na zimetambuliwa na Shirikisho la Riadha Duniani kutokana na mchango wake katika urithi wa mchezo huo.

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China

Shughuli ya Siku ya Meli ya "Xuelong 2" ya China kufunguliwa kwa umma yafanyika Hainan
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma