Kenya na DR Congo zakubaliana kurejesha uhusiano kamili wa kidiplomasia

(CRI Online) Novemba 23, 2026

Rais wa Kenya William Ruto na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi wamekubaliana kurejesha uhusiano kamili wa kidiplomasia.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotumwa na kila kiongozi kwenye mtandao wa X, makubaliano hayo yalifikiwa wakati wa mkutano wa pande nne uliofanyika Oyo, mji wa kaskazini mwa Jamhuri ya Kongo. Ruto amesema viongozi hao wawili walikubaliana kurejesha uwakilishi wa kidiplomasia katika ngazi ya mabalozi, kurejesha Tume Kuu ya Pamoja ya Ushirikiano na kuimarisha mashauriano ya kidiplomasia ya mara kwa mara. Aidha amesisitiza kuwa nchi hizo mbili pia zimeahidi kuimarisha ushirikiano katika biashara, maendeleo ya kiuchumi, usalama na utamaduni, huku zikihimiza amani, utulivu na mafungamano ya kikanda.

Rais wa DRC alisema viongozi hao wawili wamekubaliana kurejesha uhusiano wa pande mbili hasa kupitia kurejea kwa mabalozi wao, kwa moyo wa maelewano ya pande zote na kuleta amani na utulivu wa kikanda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha