Lugha Nyingine
Afrika yapiga hatua katika maendeleo ya kidijitali licha ya pengo kubwa kwenye matumizi ya Internet
Shirikisho la Mfumo wa Mawasiliano ya Simu Duniani (GSMA) tarehe 18 lilitoa ripoti ya Fahirisi ya Afrika ya Kidijitali 2026 huko Cape Town, Afrika Kusini, ikionyesha kwamba Afrika imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya kidijitali na mazingira ya sera zake, lakini bado inakabiliwa na changamoto kubwa katika kupunguza pengo la matumizi ya Internet.
Ripoti hiyo iliyotolewa katika Mkutano wa Kilele wa Afrika ya Kidijitali ulioandaliwa na GSMA, inasema mtandao wa Internet umefunika asilimia 92 ya wakazi wa Afrika, lakini ni asilimia 28 tu kati ya wanaotumia Internet kupitia vifaa vyao binafsi. Hii ina maana asilimia 64 ya wakazi wa Afrika wanaishi katika maeneo yenye mtandao wa Internet, lakini hawatumii Internet. Ili kuziba pengo hili, ni lazima kuondoa vizuizi mbalimbali. Bei kubwa ya vifaa vya kutumia Internet, ukosefu wa ujuzi wa kidijitali, pamoja na uhaba wa maudhui na huduma za kienyeji ni vikwazo vikuu kwao.
Ripoti imeonyesha kuwa kwa sasa kuna nchi 10 barani Afrika zenye kiwango ya juu cha maendeleo ya kidijitali na mazingira ya sera yaliyoboreka kiasi, ikilinganishwa na mwaka 2024 ambapo zilikuwa nchi tatu tu, yaani Kenya, Mauritius na Afrika Kusini.

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China

Shughuli ya Siku ya Meli ya "Xuelong 2" ya China kufunguliwa kwa umma yafanyika Hainan
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma