Vyombo vya habari vya China na Tanzania vyafuatilia uhuishaji wa reli ya TAZARA

(CRI Online) Novemba 20, 2026

Balozi wa China nchini Tanzania Bibi Chen Mingjian ametoa wito jana katika uzinduzi wa ziara ya vyombo vya habari vya China-Tanzania TAZARA mjini Dar es Salaam, kuwa vyombo vya habari vya China na Tanzania vinapaswa kuimarisha ushirikiano katika kuripoti kuhusu uhuishaji wa Reli ya TAZARA, na kusisitiza uwezo wake wa kubadilisha muunganisho wa usafiri wa kikanda na kuendesha maendeleo ya uchumi.

Bibi Chen amesema wanahabari kutoka nchi hizo mbili wana jukumu muhimu katika kuonesha maendeleo ya mradi huo na manufaa yake kwa umma.

Bibi Chen amesema mradi wa uhuishaji wa reli unatarajiwa kuongeza uwezo wa wa uchukuzi wa TAZARA kutoka tani laki 2 za sasa hadi tani milioni 2.4 kila mwaka, huku ukipunguza muda wa usafirishaji wa mizigo kwa karibu theluthi mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha